
Msanii Godfrey Tumaini a.k.a Ze Dudu au Baba Willy ameiambia Abby Cool & MC George kwamba, anatarajia kudondoka pande za Kaskazini mwa Tanzania, kwa ajili ya kusaka kipaji kipya katika game ya muziki wa kizazi kipya kupitia ‘talent show’ itakayofanyika Moshi, Januari 18, mwaka huu kuanzia saa nane mchana.Dudu alisema kwamba, zoezi hilo ambalo linasimamiwa na Kampuni ya Art in Tanzania lilianzia Dar es Salaam ambapo kipaji kimoja kilipatikana na sasa linaendelea Moshi, kisha sehemu nyingine itakayopangwa. “Lengo ni kuinua na kuendeleza vipaji vipya, kwani wasanii wengi wanaouwezo wa kuimba lakini wanashindwa kujua waanzie wapi”.Aidha Dudu alisema kwamba, mshindi atarekodi bure katika studio hizo na kusimamiwa na kampuni ya Art in Tanzania.
No comments:
Post a Comment