KARIBU


TANGAZO

NAFASI HII IKO WAZI KWA MATANGAZO YA MAKAMPUNI NA WATU BINAFSI WASILIANA NAMI KWA +255 737192988.

Tuesday, January 13, 2009

Dunia njia tayari inakimbiza kitaani


Dunia njia tayari inakimbiza kitaaniIle albamu ya msanii Rutta Bushoke, ‘Dunia Njia’ ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenda burudani Bongo tayari imedondoka kitaani mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanya vyema ndani ya soko gumu la muziki wa kizazi kipya.Akipiga stori na safu hii muda mchache baada ya albamu hiyo kushuka sokoni, Bushoke alisema kwamba, kila kitu kuhusu usambazaji wanafanya wao wenyewe tofauti na watu wengi walivyozoea kwamba kazi hiyo huwa inafanywa na ‘Wadosi’.“Dunia Njia ina jumla ya nyimbo kumi na moja, ukiwemo ‘Usiende Mbali’ ambao nilishirikishwa na Juliana wa Uganda, nimeuingiza kwenye albamu yangu ili kuwapa ladha zaidi mashabiki wangu. Kwa kifupi ni albamu ambayo haisimuliki, unachotakiwa kufanya ni kuinunua na kuisikiliza,” alisema Bushoke.Ngoma nyingine zinazopatikana ndani ya albamu hiyo ni pamoja na Chupa ya Coca’, Nimekuchagua wewe, Nimeshafika, Mapenzi Yaongee na nyingine kibao

No comments:

Post a Comment