KARIBU


TANGAZO

NAFASI HII IKO WAZI KWA MATANGAZO YA MAKAMPUNI NA WATU BINAFSI WASILIANA NAMI KWA +255 737192988.

Tuesday, January 13, 2009

Dark Master Kuwafuata wana Chamber kileleni


Kutoka ndani ya familia ya Chamber Squard ambayo inaundwa na ‘membaz’ kama Ngwea, Noorah na Mez B, msanii Athumani Hamisi a.k.a Dark Master anatarajia kuwafuata wenzie hao kileleni baada ya kukamilisha ngoma zake kadhaa zitakazoibeba albamu yake mpya yenye jina la ‘Mtoto wa Chimwaga’.Mchizi ambaye amefanya maajabu kanako korasi ya ngoma, ‘Nipe Dili’ ya kwake Ngwea, amesema kwamba, kitu kikubwa kilichomfanya achelewe kutoka kama wenzie ni kutopewa nafasi na wadau japo uwezo wake uko juu katika game ya muziki wa kizazi kipya, lakini hivi sasa wameshamkubali na kinachfuata na kazi tu.Dark ambaye pia alifanya vyema kunako nyimbo nyingine kama ‘She Got Gwan’ wa Ngwea na ‘Part ya East Zou’ aliyoimba na kundi lake hilo na nyingine alisema na ShowBiz kwamba, kupitia studio za Backyard Records, tayari ana mawe kibao ambayo yataanza kwenda hewani siku si nyingi kwa ajili ya kuitambulisha albamu hiyo ambayo iko tayari. “Ndani kuna kazi kibao zikiwemo, Azimio, Bakora, Kalinga Chibite na nyingine, pia nimewashirikisha wasanii kama Prof. Jay, Sugu, Ngwea, Bushoke na wengine,” alisema.

No comments:

Post a Comment