KARIBU


TANGAZO

NAFASI HII IKO WAZI KWA MATANGAZO YA MAKAMPUNI NA WATU BINAFSI WASILIANA NAMI KWA +255 737192988.

Tuesday, January 13, 2009

Sauti ya Ghetto


Bila shaka utakubaliana nasi tukisema kwamba viwango vya ubora wa video za miziki kutoka Tanzania vimekuwa vikipanda siku baada ya siku.Siku hizi video nyingi zinakuwa zinaonyesha sio tu uhalisia bali pia zinabeba maudhui mazima ya nyimbo husika.Kwa hilo ni lazima tuwapongeze wasanii na pia waongozaji au watengenezaji wa video hizo.
Hali hiyo ndiyo tuliyoishuhudia hivi karibuni tulipotembelea kambi ya Prof.Jay wakati wa kutengeneza video yake ya wimbo Sauti ya Ghetto ambao umekuwa ukikamata mawimbi ya radio nchini Tanzania kwa muda sasa.Video hiyo inatarajiwa kutoka rasmi mwishoni mwa wiki hii

No comments:

Post a Comment