
VIKAO vya kutetea maslahi yao wasanii wachekeshaji vimeendelea kufanyaka katika ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni, jana jumapili katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wachekeshaji wengi kiliwaarika wasanii wakongwe pamoja na Rais wa Shirikisho la Wasanii (TAFF) Simon Mwakifwamba (Gasper) na Mwenyekiti wa kundi la Kaole Sanaa Group Salum Mchoma almaarufu kama Mr. Chiki.
Kingwendu, Augustino Robert, Mtanga.
Lengo likiwa ni jinsi gani wataweza kupata maslahi zaida katika kuuza kazi zao za vichekesho sawa na filamu kwani kazi zao nyingi zimekuwa hazithaminiwi kwa sababu ya mfumo uliokuwepo wa kuwa waigizaji hawa ni watu wasiohitaji malipo ya zaidi na hata kazi zao zinaonekana kama ni kazi zilizokosa maandalizi kutokana na muonekano wao.
Akiongea na fc mmoja wa wageni hao bwana Chiki alisema kuwa wasanii ni lazima wabadilike katika maandalizi ya kazi zao kwani bado kuna masihara katika maandalizi ya komedi hizi na kuwa kazi mbovu na pengine hata kupoteza thamani ya kazi hii na wasambazaji kuona hakuna faida katika kununua kazi hizi.
.
Chiki Mchome Mwenyekiti Kaole Sanaa Group
“Nimekuja hapa katika kikao hiki lakini inawezekana kuwa maneno nitakayoongea yanaweza yasiwafurahishe kabisa na si lengo langu mfurahi zaidi ya kuelewa, nasema kwanza sifurahii hilo jina la kujiita makomediani tafauteni jina lingine, jambo lingine mbadilike siyo kuchekesha lazima mvae miwani ya ajabu ajabu, maandalizi ya komedi ni rahisi sana mtu anakuja anasema kimbia anguka tayari eti kichekesho!!” Anasema Chiki.
Naye Rais wa Shirikisho la Wasanii alisema kuwa mabadiliko na mapinduzi si jambo la mara moja kwani wakati watu wakijaribu kufanya hayo mapinduzi na watu wengine wenye maslahi binafsi utumia njia nyingine katika kuhakikisha kuwa wanamapinduzi wasiendelei kupambana na kupata maslahi yao katika kuleta maendeleo yao katika kazi wanazofanya.
“Jamani huku kuna vita kubwa kuhusu maslahi ya wasanii, ni wasanii wachache tu ndiyo wanaoonyesha kuwa wanapata maslahi na si kwa wasanii wote kitu ambacho ni tatizo kwa jamani amkeni na kuungana kwa ajili ya kudai maslahi, kwa sasa hali si nzuri katika tasnia ya filamu na kazi nyingine kwa jumla” Anasema Rais wa TAFF.
No comments:
Post a Comment