KARIBU


TANGAZO

NAFASI HII IKO WAZI KWA MATANGAZO YA MAKAMPUNI NA WATU BINAFSI WASILIANA NAMI KWA +255 737192988.

Friday, January 16, 2009

JUMA NATURE ATAMBULISHA SINGO YAKE MPYA


Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Sir Juma Nature leo mchana amefanya utambulisho wa wimbo wake mpya uitwao ULEVI kutoka kwenya albamu yake mpya ya tano inayoitwa TUGAWANE UMASIKINI yenye jumla ya nyimbo kumi.
Mmoja wa wasaniii wa karibu wa msanii huyo,Rich One ameiambia JIACHIE leo mchana kuwa wimbo huo wenye mabadiliko makubwa tayari umekwishasambazwa kwenye vituo kadhaa vya redio mbalimbali za hapa jijini Dar na kwingineko.
"Kwa hiyo leo tunaanza utambulisho wa singo ya kwanza inayoitwa ULEVI,ikiwa kama utambulisho wa albamu hiyo iliyorekodiwa ndani ya studio za Bongo Records chini ya prodyuza mahiri P-Funk, na albamu kuanzia wiki ijayo itaingia sokoni tayari kwa mauzo"amesema Rich One
Aidha Rich One amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Ulevi,Ofisa Usalama,Siku za wiki,Nimeshakwama,kukakaa maskani,Burudika,nitakuwa mgeni wa nani na wimbo wa kilichokusibu.
.Juma Nature mpaka sasa amekwishatoa albamu nne ambazo kiukweli zilitamba na kukubalika vilivyo katika anga ya muziki wa bongofleva, albamu hizo ni Nini Chanzo,Ugali, Ubinadamu kazi pamoja na albamu ya Historia

No comments:

Post a Comment